BLIND GIRL’S LOVE (PENZI LA MSICHANA
KIPOFU)
Neno penzi kila mmoja analichukulia kwa uzito wake na kwa namna na huwa
haliingiliwi na mtu mtu zaidi ya wapendanao.
kutana na kijana Imma aliyejikuta kwenye penzi la
binti kipofu (Salma) mrembo mwenye umbo la kuvutia na sauti iliyolaini yenye
kubembeleza ambaye hayuko tayari kusikia neon Mapenzi kwenye maisha yake kutoka kwenye familia kimasikini, huku wazazi
wake imma wakimpinga kipofu huyu kwa kudai kuwa na mahusisano na kipofu ni
mkosi kwenye familia hasa ya kitajiri kama yake.
Huku wakimlazimisha kuwa na uhusiana na Rose binti
kutoka kwa mzee Martini Tajiri maarufu mkoani Tanga.
Mmmmmhhhh
nini ktatokea?
Je Imma anaweza
kupangiwa mtu wa kuwa nae na hata akiwa na Salma wakati wazazi hawako radhi,
maisha yao
yatakuwaje?
Fuatilia
hadithi hii tamu yenye kufunza na kusisimua kuazia sehemu kwanza hadi ya mwisho
kila wiki kutoka Kwa mtunzi wako MR.Njama.
SEHEMU YA KWANZA
Ni asubuhi Mwanana ndani ya jiji la tanga nyumbani kwa kina
Imma Salimu mlango unagongwa na mlinzi anafungua. Ulikuwa ni msafara wa magari
yasiyopungua matano na wageni wanaingia ndani ya jumba la kifahari la mzee Mwanjala
liiloko barabara ya irishihni na moja katika jiji la Tanga nchini Tanzania ,
mara baada ya salaam Mzee mmoja anaonekeana kuongea kwa sauti ya chini na Mzee
Mwanjala kasha mzee Mwanjala anaamuru Imma aitwe.
je ni wakina nani na
wanashida gani na Imma? endelea………………
Ulikuwa msafara wa Mzee Martini ambae alikuwa mfanyakazi wa
bandari ya tanga na baada ya kustaafu
anapewa pensheni yake,ni Mzee wa makamo kidogo mwenye mtoto mmoja tu wakike aitwae Rose.
Imma anaamka na kukuta watu wamejaa kwao pembeni anamuona
msichana mrembo anaemfahamu si mwengine
bali ni Rose Martini.
Imma ni kijana mwenye umri wa miaka ishirinina na mbili
aliyepata elimu yake ya msingi katika shule ya msingi Future Light iliyomo tarafa ya Maramba mkoani Tanga
na kufanikiwa kwenda Sekondari Mkwakwani ambako alipata elimu yake hadi
kidato cha sita na kufanikiwa kwenda
chuo che elimu ya biashara (cbe) kilichoko jijini dar es slaam baada ya kupata
Degree yake ya kwanza ya biashara anapelekwa nje ya nchi kuchukua Digrii ya
pili nchini Canada akiwa huko anakutana na Muafrika mwenzie sio mwengine bali
ni msichana Rose Martini kama ilivyo kawaidia kwa uatamaduni wa wa Afrika
wakutanappo nje huwa kama ndugu lakini hwa ilikuwa tofauti kwani kilammoja
alionekana kutomjali mwenzanke ingawa Imma alitamani sana wafahamiane
Baada ya kuchuniana
kwa muda wa wiki mbili tangu Rose na Imma wakutane kwenye chumba cha kulia
chakula. ingawa Imma alionyesha kumjali Rose Lakini Rose alizidi kujiona kama
hata hahisi kama Imma ni mwa afrika mwenzie kwani alikuwa busy muda wote na marafiki
wa kizungu na kumuona Imma kama mluga luga Fulani baada ya wiki mbili kuisha
Imma akiwa kwenye bustani ya kupumzika hii ni baada ya kuchoshwa na masomo kwa
mbali anamuona msichana huyo mrembo Rose anakuja huku akiwa na bia mbili
mkononi.
Hi bro? aanza kwa kumsalimia Imma
Hi how are you? anajibu Imma.
Am doing fine are you from Africa ?
anauliza Rose
Yes iam anamjibu
Imma.
wow which country please? anaendelea kuuliza Rose huku akiwa
anakaa kwenye bustani hiyo akiwa na kisket kifupi huku nguo ya ndani ikiwa nje
huku akiamini kabisa Imma atakuwa anaiona.
No you can not be
serious are real Tanzanian? That my country am also from there anajibu Rose
huku akionesha kutoamini kwa dhati kuwa Imma ni Mtanzania mwenzake.
can you speak
Swahili? anauliza Rose.
yes I can anajibu
Imma kwa kujiamini.
ok lets make it anamalizia Rose kwa kumuomba sasa waongee
kinyumbani.
Mbona uko peke yako
hapa bustanini? aliuliza Rose.
Yaa huwa napenda kukaa peke yangu ingawa pia sina kampani,
alijibu Imaa kwa style ya kuchombeza huku jicho lake likiwa
kwenye mwili wa Rose mmmhhhh.
Mhhhhh huna kampani au huzitaki’’ kabla Imma hajajibu
anadakia tena Rse ‘’
Unakumbuka ,mara ya kwanza tulipoonana nilitamani
sana kuwa karibu na wewe ila nikagundua uko
Serious sana .
‘’hapana mbona wewe ndio ulionyesha kuwa Serious’’ akajibu Imma ‘’ okey
tuachane na hayo mimi naitwa Rose Martini nina mwaka wa pili chuoni hapa
nimetokea Tanzania Mkoani Tanga ninachukua Degree ya kwanza ya udaktari sijui
mwenzangu’’ alijieleza kwa kujiamini sana
mrembo huyu Rose.
‘’mimi naitwa Mr:
Imma Salim nafurahi kukufahamu sio tu ,kwakuwa mtanzania mwenzangu bali mtanga
mwenzangu ninachukua Digrii ya pili biashara
na nina miezi mitatu tu chuoni hapa’’alijieleza Imma.
Nashukuru sana
kukufahamu au kufahamiana na wewe unjua ni vigumu kukutana na mtu wa nchi mmoja
nje yam chi mara nyingi huwa ni bara moja au hata nchi moja anaendelea Rose.
huwa unapendelea kukaa maeneo gani hapa chuoni maana last
time nilikuona canteen la leo hapa, aliuliza Rose.
Huwa napenda sana
hapa vipi unaishi ndani ya chuo au umepanga nje? aliuliza Imma.
No naishi humu humu chouni mimi maisha ya nje ya chuo
nayapenda sana
ila Baba hataki hata kusikia.alijibu Rose.
ok sasa vipi ngoja
nikakuchukulie bia alisema Rose huku anaamka.
Hapana kwa kweli sijawahi kunywa bia na sifikirii kama nitakuja kunywa hata siku moja
lakini pia huu ni muda wa mzaoezi naomba nienda tutakutana
tena alijibu Imma huku akiamka.
poa ucjali naweza pata namba ya simu maana tumeshakuwa ndugu
sasa. anamlizia Rose kwa kuomba namba ya simu pia ningependa unipe ramani,
anuani na hata namba ya wazazi wako ili tukifika Tanzania
tuwasiliane pia aliomba mrembo Rose kwa jinsi alivyoumbikani wazi kwamba kama
akiamua kugombea umiss basi Tanzania
tunashinda miss World.
Kwani kuguo chake
kifupi na mapaja yake malaini yalozungukwa na tite nyeupe yakiwa wazi huku
akiwa amevaa kishati cjha kubana chenye kuonesha mzaiwa yalochomozea kama nchi ya bamia yakiwa yanaonekana kwa juu na ndani
kwani shati lilonesha kila kilichoko ndani.
Mmmmmmhh Imma atafanyajeee endelea jumaapili ijayo hapa
kwenye hii blog yetu.
Unaweza toa maoni
yako pia.
SEHEMU YA PILI
Imma alimpatia namba na ramani kama alivyoomba huku
akichukuka za kwake kwa nia ya kudumisha mawasiliano kama
ndugu.
Kwa muda mfupi tu Imma na Rose waliweza kuzoeana na
kupeana faraja kwa kutembelea sehemu tofauti.
Ingawa hii ilimfanaya Imma kujua maovu ya Rose kwani kwa
kifupi ni mrembo anaependa sana
starehe.
Weekend ya tatu
toka wafahamiane Rose alimuomba waende Night Club’
Rose” can you take me to flash night club please”
Mmmhhh its ok even if am not used to,but I will,don’t
worry coz I don’t mean to borther you. Alijibu Imma.
Ilikuwa ni ujumbe mfupi wa simu (sms) kutoka kwa Rose.
siku hiyo usiku Rose alivaa skin jeans nyeupe na t-shirt
black huku mguu akiwa na kicheni cha gold,kiunoni alikuwa na cheni ya gold,
T-shirt yake haikuweza kuficha kile kilichopo kiunoni.
Huku umbo lake la namba nane na pisto za mapaja kama
zinataka kupasua skin jeans huku akiwa anaelekea kwa Imma.
Imma am out please can we go ilikuwa ni sauti ya mrembo
Rose akiita nje pembeni kidogo na moja ya dirisha la nyumba zakuishi wanachuo
ambapo imma alikua akiishi, “ok come in am just to finish” ilikuwa sauti ya
Imma, baada ya muda Rose alikuwa ndani. Ok nipe kama dakika tano please aliomba
imma huku Rose akitingisha kichwa kama ishara
ya kukubaliana na maombi hayo.
Mmmmmmhhhh huyu dada jamani mtihani huu nitafaulu kweli?
Alijiuliza imma kama ishara ya kuchanganyikiwa
na mavazi na umbo la mrembo Rose usiku huo.
“Ok how do we go” aliuliza Rose, we will use my bike
alijibu imma.
Mmmhh no please is not safe why cant we use tax please?
alichangia Rose.
No lets use bike its simple,safe and flexible.
Ok we will don’t worry imma alikubali Rsoe.
Alitoa pikpiki aina ya BMW ambayo huitumia kwenye
mizunguko ya ke ya hapa na pale mjini, Rose alipanda huku kiuno chake chenye
cheni ya gold kikiwa wazi huku umbo lake
nikidhihirisha uwezo wa
Mwenyezi mungu kwenye uumbaji..
Ilikuwa ni safari ya zaidi ya dakika kumi kwa mwendo wa
kawaida sana huku safari yao
ikitawaliwa na stori za Tanzania .
“Can you take some bear please”? ni sauti ya Rose muda
mfupi baada ya kukaa kwenye kwenye meza iliyoko pembeni kidogo na mwanga
ulokuwa ukimulika kwa kufifia na huenda ndo sababu ya kuitwa ukumbi huo flash
night club ilioko jiji la Ottawa ,eneo la 400
dalhousie kati ya besserer na Rideau nchini canada
ambao hufunguliwa
kila ijumaa na jumamosi tuu,kuanzia saa tatu ucku hadi kumi asubuhi.
“Thanks Rose am not tarking alcohol” huku akiagiza maji.
Baada ya maongezi na muzik wa hapa na pale siku ilionekana
kuwa nzuri sana kwa Rose hasa baada ya kupata kilevi,ingawa kwa imma ilionekana
ya mawazo sana kwani hakupanga kuwa na msichana akiwa masomoni lakini kwa pozi
za Rose mmmhh akili ilianza kubadili mawazo.
“Please I don’t feel like going there my self please lets
finish a day” mmmh ilikuwa ni sauti ya Rose huku akiwa amemkubatia Imma kwenye
bike (pikipiki) wakati anakatisha kumpeleka kwake kuku wakiwa hoi kwa mziki ni
pilika za club
What wwhhat do you mean Rose? Aliuliza Imma.
I mean take me to your place please we have been together
from that time please lets close the day with destiny of our happiness. Alikazi
Rose huku akionekana kuwa serious kwa kile anachokisema.
Imma alitafakari kwa kina kuhusu ombi lile huku akiamini
amefanikiwa kumbeba temba kwenye bajaji,kisha akaona ni heri kwake huku akijawa
na uchu wa kumpata mrembo huyo kiulaini
Mmmmhhh please can we go together my best,No please just
do it first then I will after, ilikuwa ni malumbano baada ya kufika kwa Imma
huku Rose akikataa kuoga peke yake.
Imma inahisi anaua tembo kwa ubua lakini ghafla Rose akiwa
bafuni simu yake inaingia sms,ghafla Imma anapata hamu ya kuifungua ghafla
anapigwa na butwaa “Sweetie I saw you with African its your time to give others
as you gave it to me, but note that you have distructed my life and my
strengths are no longer as before, am dying just because of you,good night”
ulikuwa ujumbe mfupi ulosaviwa kwa jina la Never.
Its you now, unaju yale maji ni baridi hadi pombe yote
imekwisha ilikuwa sauti ya Rose huku Imma akiwa hana raha kwa ujumbe tena muda
huu wa usiku.
I dont feel like eating anything am full lets us sleep ni
sauti ya imma baada ya Rose kudai ameshiba ila nataka Imma ale,
Alivua taulo taratiiibu na
kupanda kitandani huku mziki ukisikika kwa mbali lakini Imma amejawa na
mawazo,mmmmh are you ok imma?
for sure am not may be because of dancing alijibu imma
kuku akiwa hayuko tayari kumueleza nini kimetokea.
rose aliishika simu yake na ghafla akaona ile messahe
ikiwa imefunguliwa .
aliisoma kwa makini sana kisha huku imma akimuangalia kwa
jicho la pembeni ili kuweza kugundua lugha ya sura yake baada ya kuisoma kitu
kilichomchanganya zaidi ni kwa Rose kutostushwa na sms ile zaidi ya kuisoma na
kuidharau kwa kukunja mdomo kisha akaizima na kuiweka pembeni huku akimtaka
Imma amlalie kifuani.
no no no Rose i can live live like this? alifoka ImMa huku
akiamka na kukaa kitandani.
kwani ni nini Imma mbona sikuelewi au ni hii sms ya huyu
mpuuzi ndo inakuchanganya?
mpuuzi mpuuzi aje weakati jamaa anakufa? alijibu Imma kwa
kufoka.
"anakufa ndio si anakufa kwa ujinga na atamaa
zake" alijibu Rose huku akigeukia upande wa pili wa kitanda huku
jibu hilo
likizidi kumchanganya akili.
tafadhali Rose naomba amka ulieleze kwa upanda
unachomaanisha, alianza kuwa mdogo na kuongea kwa sauiti ya chini.
no no no imma nimechoka tafadhali naomba uniache, hebu
tulale tutalongea hii mada kesho.
Nini kitaendelela je
kunalalika na nini kimejificha kwa Rose na Imma anawza nini?
usikose sehemu ya tatu ya
hadith hii yenye ukweli ndani yake.
Pia unaweza kutoa mawazo au
swali.
Mungu ndo mwangaza wetu kwa
kila jambo.
SHEHEMU YA TATU:
SHEHEMU YA TATU:
No no no Rose i can live live like this? alifoka Imma huku
akiamka na kukaa kitandani.
kwani ni nini Imma mbona sikuelewi au ni hii sms ya huyu
mpuuzi ndo inakuchanganya?
mpuuzi mpuuzi aje weakati jamaa anakufa? alijibu Imma kwa
kufoka.
"anakufa ndio si anakufa kwa ujinga na atamaa
zake" alijibu Rose huku akigeukia upande wa pili wa kitanda huku jibu hilo likizidi kumchanganya akili.
tafadhali Rose naomba amka ulieleze kwa upanda
unachomaanisha, alianza kuwa mdogo na kuongea kwa sauiti ya chini.
no no no imma nimechoka tafadhali naomba uniache, hebu
tulale tutalongea hii mada kesho.
“Hapana naomba uniweke wazi juu ya suala hili” aliendelea
kuhoji Imma.
Huyu jamaa anadai ananipenda sana
na kamwe hawezi kuishi bila ya mimi ni kijana kutoka Nigeria na nmemeshamwambia kwamba
hatuwezi kuwa pamoja, alieleza kwa ukali Rose.
“but you talk hukuwahi kuwa na uhusisanao na ilikuwaje jamaa
anakusumbua hivyo na ujasiri gani ulikufanaya kutokuwa nae”?
Try to understand Imma I just don’t need the guy that all,
please lets get sleep am tired.
Ok your wish is my command lets sleep but nothing I can with
you this night unless I know the truth.
“Its ok lets sleep I can’t ague with you just because I love you imma”
Imma hakuwa na amani kabisa kiasi cha kukosa hata hamu ya
kufanaya tendo na Rose kwani ile sms ilimfanya awaze usiku mzima huku akiamini
Rose anasiri kubwa kuhusu yule jamaa.
Mahusisano
yaliendelea ingawa Imma alihakikisha hawaliendei tendo la ndoa.
Ndani ya uhusiano wao Imma aligundua mengi kuhusu Rose
ikiwemo tabia yake ya kujichanganya na wadada waloshindikana chuoni hapo huku
akitoka na wanaume wa aina tofauti ingawa hakuwahi kukubali hilo mbele ya imma,huenda ni kwa kuwa
alimpenda ndo maana aliogopa kumpoteza.
Miezi mine mbele Rose alimaliza mitihani yake ya mwisho na
kurudi Tanzania huku
akimuacha Imma nchini Canada .
Akiwa Tanzania Rose aliomba kazi kwenye Hospital
iliyoko ndani ya mkoa wake wa Tanga kwani hakupenda kuwa mbali na wazazi wake
ambao aliwamisi kwa miaka kadhaa.
akapata kazi kwenye hospital ya Bombo mkoani hapo akiwa anamawasiliana
na Imma kupitia kwenye email na simu,huku akiendelea kumuomba avumilie kwa
kumhakikishia kuwa yeye yuku Tanzania
na hawezi kuwa na mtu hadi yeye atakaporudi.
Mkaisha ya Rose jijni Tangu aylikuwa mazuri kwani alikuwa
akilipwa vizuri achana na ukweli kwamba familia yake ilikuwa ikijiweza
kiuchumi.
Alijitahihdi kudumisha mawasiliano na Imma hadi Imma
alipohitimu masomo yake..
Baada ya
mwaka mmoja na nusu Imma alikuwa ameshamaliza masomo yake nchini Canada na sasa
inabidi arudi nchini Tanzania, mapokezui ya Imma yalifanywa kwa siri sana na
Rose kwani alitoka tanga na usafiri binafsi na kumfuata Imma jiji dar kisha
akampeleka hoteli maeneo ya magomeni mapipa ijilikanayo kwa jina la New Bondeni hoteli,kitu kilichomshangaza Imma
ni pale Rose alipomkataza hata kuonana na Rafiki yake wa karibu Iqram
Imamu ambae baada ya kuhitimu wote chuo
cha elimu ya bishara (cbe) alianzia ofisi inayojihusisha na ajira za walimu
hapa Tanzania Teaches’ Junction iliyoko maeneo ya hapo hapo magomeni huku
akidai kwamnba amechoka hivyo anapaswa kupumzika, asubuhi alimchukua na
kumpeleka moja kwa moja Tanga.
Wakiwa tanga walikuwa karibu kaka
marafiki wa wakaida.
Baadaa ya miezi mine kupita Imma huku akifanya jitihada za
kutafuta ajira kwenye maofisi mbalimbali mwishowe alifanikiwa kupata kwenye
kampuni kusafirisha mbao nchi za nje
iliyoko mkoani Tanga Costal Forest Trade akawa anafanya kazi kama
meneja wa usafirishaji kwenye kampuni hiyo.
Baada Mwaka mmoja
kazini hapo huku kila mara rose anakuja nyumbani kwao na wakati mwingine
walikwenda wote Club Lacasa kujirusha lakini Imma alijitahidi sana kumshawishi
Rose ampe ukweli wa ile sms lakin Rose
alishikilia msimamo wake kwamba yule kaka alikuwa akimtaka nae hakuwa tayari,
ingawa imma aliamini kuwa huenda Rose ni Muathirika wa virusi vya ukimwi kwa
tabia zake na ile meseji vilimpa picha tofauti hivyo kuamua kiume kwamba hawawezi
kuwa wapenzi hata siku moja.. Mwaka mmoja
baadae wazazi wa Imma
wanamgusia mtoto wao kuoa na kumwambia kwamba itabidi aishi na mkewe hapo hapo
kwao ingawaje swala la kuoa kwake haikuwa tatizo kwani alikuwa akilipwa
mshahara mzuri tu kwenye kampuni hiyo na kumsisitiza kwamba ni vyema kama anamtu anethani anafaa amlete nyumbani.
“ni muda sasa
umepiata Imma mwanangu sijui una mawazo gain juu ya sula ya kuoa?” ilikuwa ni
kauli ya Baba yake mzazi.huku mama akiwekea mkazo,huu ulikuwa muda mchache tu baada
ya chakula cha usiku.“Tena
kwakuwa mmeshaguana ni vyema tumite tuu
mzee martini tujue nhini kinafuata”
Mmmhhh mama? Imma alishangazwa sana na kauli ile huku
akipata picah kuwa wazazi waliamini kuwa
wao ni wapenzi , huku wakiteka amuoe mototo wa tajiri mwenzao ili waishi maisha
ya kifme baada ya kusikia taarifa hizo Imma anakataa kata kata na kudai Rose ni
rafiki yake na kamwe hawezi kuwa mkewe, ila kwa upande wa wazazi hakuweza
kumuelewa hukuwa wakidai kwamba tabia yake inaridhisha kwani hakuwahi kusikia
tabia mbaya yoyote hapa jiji kabla na baada ya kwenda chuo na hata baada ya
kurudi.
No imma don’t disappoint our family,sikotayari umuoe
mwanamke mwingine yoyte mbali na Rose tafadhali mwanagu. Hii ilikuwa kauli ya
mama yake imma.
“Mom but she is not my ideal? How will I marry whom I am not in love with”?
Alihoji imma kwa sauti ya mshangao,
“Lsten to your mom
imma we have discussed these things before here and all what you have as an
obstacles we thought about before telling you, so please get ready for
Mr.Martin Daughter I real respect my friend I will never disappoint him, this
is my last say to you” aliongea maneno hayo makali hkukakiamka na kwenda ndani
huyo alikuwa mzee mwanjala ambae pia alifahaika Tanga kwa misimamo ya kauli
zake.
Ilikuwani kauli
nzito sana
ilomfanya imma kukosa jibu huku akiwa amepewa siku mbili kutoa msimamo wake juu
ya kumuoa binti huyo.
“ Am not happy
with my life anymore,I cant disappoint
my parents but I cant live with Rose I don’t love her at all,how will i live
with her”ilikuwa ni kauli ya imma akimueleza james ambao walikuwa wakifanya
kazi ofisi moja.
Ok my lovely parents I real respecting you but ………………………….
Endelea kufuatilia hadithi wiki ijayo kwenye sehemu ya nne.
Nini kiatokea na nini penzi la kipofuuuuuuuuuuu
Unaweza pia kutoa maoni yako kwenye hapo hapo kwenye comment.
mungu ndo mwanga wa maisha yetu.
SEHEMU YA NNE
mungu ndo mwanga wa maisha yetu.
SEHEMU YA NNE
Kwa kuwa wazazi walilazimisha imma
hakuona sababu ya kuendelea kuwapinga wazazi wake ingawa kwa upande wake hakuwa
tayari kwani historia ya Rose alikuwa akiifahamu kabla.
“Ok mum as I told you I will but
mind you this is not my decision, I gave you answer but you just think twice
about this,getting married is my right and whom to marry is my right too”.
Alitoa jibu hilo
kwa sauti ya ukali huku Baba ayake na Mama wake wakibaki wakitazamana kama kutoamini kile kinachotoka kwenye kinywa cha mtoto
wao kipenzi.
swala la kuoa kwake halikuwa tatizo kwani
alikuwa akilipwa mshahara mzuri tu kwenye kampuni hiyo tatizo ni kwanin
walitaka lazima amuoe Rose mtoto wa tajiri mwenzao ili waishi maisha ya
kitajiri wakati yeye anaamini hata bila ya kufanya hivyo tayari angeweza kuishi
maisha mazuri tena kwa msichana ampendae
Shikamoo mzee’’ anasalimia Imma huku akiwaza kuhusu ujio wa wgeni wale,ulikuwa
ni msafara wa wazee wapatao ishirini ambao kwa hali ya kawaida walionekana kuwa
na hadhi ya juu ingawa imma alifanikiwa kumuona mmoja tu wakati anafungua
mlango wa chumbani kwake akitokea store ya magari, akiwa kwenye mawazo “kaka
imma,kaka imma” ilikuwa ni sauti ya mfanyakazi wa ndani ikimjuza kuwa alikuwa
akiitwa na mzee sebuleni, hapo hofu inaanza kumjia, “ina maana wameshindwa
kabisa kufikiria juu ya ukati;I huu ok but I cant marry Rose”yalikuwa mawazo ya
imma yakijirudia kichwani mwake baada ya kuitwa.
‘’Imma natumai unamfahamu huyu binti na huyu
ni Baba yake anaitwa Mzee Martini Hizza na hawa wengine ni ndugu zako utawafamu
taratibu lengo la kuja hapa ni kuhusu uchumba na harusi kati yako na Binti yao
Rose hivyo naomba uiwasalimu ili tuweze kuendelea ’’alimaliza mzee Mwanjala
baada ya maneno hayo mrembo Rose alitoa tabasamu la hali ya juu lakini kwa
upande wa Imma hakuonyesha kufurahi bali kujikuta akitetemeka kama mwanaume
anaetaka kuozwa ndoa ya mkeka kwani Rose hakuwa chaguo lake.”hatuoni sababu ya
kuchanganya familia tusizo zifahamu unajua familia nyingine ni matatizo unaweza
kuoza binti ukashangaa mali
zako zote zinatoweka” yalikuwa maneno ya mzee Martin,
Ok unaweza kwenda na huyu binti
pia kwani hafuatayo hapa hayawahusu baada ya kusiskia maneno hayo aliamka
nakwenda moja kwa moja hadi chumbani kwake na kujifungia hiyo ilikuwa ni kauli
yam zee mwanjala mzee anaesifika kwa misimamo ya kizamani.
Baada ya kikao hicho sasa Imma na Rose
walikuwa wachumba,kila siku wakawa wanakutana na kuzungumzia maisha yao wakiwa kama mke na mume watarajiwa wakiwa wameshapanga
ahadi ya harusi yao
je.
Imgawa kwa upande wa imma hakuwa akiifurahia
ndoa hiyo huku akiwaza kutoroka nyumbani wazo ambalo huvurugiga tu baada ya
kumkumbuka mama yake kipenzi Salama hivyo kujikuta akiingia kwenye maamuzi pasi
na kuridhia.
Mwezi mmoja kabla ya harusi ya
kitajiri kila kitu kilikuwa tayari na kila pande ya jij hilo la Tanga ilikuwa
na taarifa juu ya harusi hiyo ambayo inasubiriwa kwa hamu na wakazi wa Tanga
ili kuona nin kitafanyika kwani mzee martini aliahidi kushanga jiji hilo kwenye
harusi ya binti yake kipenzi.
Imma akiwa ndani ya gari yake ya kazini aina ya Rava 4 kwenye makutano ya barabara za kisosora na
stendi kuu ya jiji hilo
lilobarkikiwa kwa viwanda na kilimo.
Ni majira ya saa kumi na moja
joini akiwa amechoka kwa kazi za siku nzima huku kichwa chake kikitawaliwa na
mawazo mfano wa mama alopoteza mume,nyumba,kazi na watoto kwa wakati mmoja akiwa anatoka kazini kuelekea nyumbani anajikuta
kifunga breki za gafla baada ya msichana mmoja kupita karibu na gari huku akiwa
speedi ya stini anafunga breki ya ghafla huku akijikuta akitekemeka mara
anashuka huku akiwa ametawaliwa na hasira kali kwa lengo la kumpiga huku akiwa
anafoka ‘’mmpumbavu mkubwa kwanini Unataka kunisababishia ajali ina maana
hunioni na hata ungurumo wa gari huusikii au ndio mnataka madereva tuwapishe
ninyi?’’ilifoka kwa hasira kuhu akiwa amepaki vibaya na kusababisha foleni ya magari yapatayo thelathini .
‘’ naomba unisamehe kaka mimi sioni na wala
wala sio kosa lako naomba nisamehe kaka’’ ni sauti ya msichana akiwa ameshika
fimbo alioashiria kuwa ni mlemavu wa macho (kipofu) akiomba msamaha huku akilia
kwa uchungu huku akikimbia kando ya barabara huku akipapasa papasa na kifimbo
hicho.
Imma alishusha pumzi na kumuomba msamaha
yeye ‘’sikufahamu dada naomba nisamehe kwa kukufokea, imma alirudi kwenye gari
na kupaki vizuri ili magari mengine yapite kasha akarudi kwa yule binti ambae
alikuwa pembeni akilia huku akitetemeka “binti naomba unisamehe tafadhali najua
unavyojisikia tafadhali sikuwa nafahamu hali yake naomba twende kwenye gari nikupeleke
unakoelekea tafadhali’’ sio siri Imma alimuonea huruma sana ‘’samahani kaka nisikupotezee muda nashukuru
kwa kunisamehe kwani huenda unge sababisha ajali na kuharibu maisha yako pia
nashukuru kwa roho yako ya huruma ila naomba uende tu ‘’ Imma alitamani kulia
nakujutia hasira zake na wala hakuwa tayari kumuachia alimbembeleza lakini hakuwa tayari kupanda
kwenye gari huku akiomba imma amruhusu aende nyumbani kwani yeye ndo mwenye funguo.
“ingawa huko tayari kuniruhusu
nikupeke basi hata jina lako na wapi unaishi tafadhali”
Hapana kaka tafadhali naomba
usinidhuru tena sina sabau ya kukupa jina langu wala wapi na kaa tafadhali
naoma niache niondeke alisema binti.
Wakati imma akiwa amemshika mkono
akimbembeleza asilie kwa mbali anaona gari ya Rose ikwa inakuja kwa speed kali
kuelekea aliko imma.
Mmmmmmmhhh nin kitafuatia yule Rose anakuja kufanya nin na kwanin yuko
speedi kiasi hicho……………………………………..??????.
usikose sehemu ya tano ya hadithi hii yenye ukweli ndani
yake.
Unaweza pia kutoa maoni yako kwenye hapo hapo
kwenye comment.
“mungu ndio mwanga wa maisha yetu”
SEHEMU YA TANO
Hapana kaka tafadhali naomba
usinidhuru tena sina sabau ya kukupa jina langu wala wapi na kaa tafadhali
naoma niache niondeke alisema binti.
Wakati imma akiwa amemshika
mkono akimbembeleza asilie kwa mbali anaona gari ya Rose ikwa inakuja kwa speed
kali kuelekea aliko imma.
Mara imma akastuka kuona gari ya
Rose ikiwa speed kuelekea walipo, ila ghafla gari ile iliwapita kwa speed ile
ile ndipo imma aligundua kuwa aliekuwa akiendesha hakuwa Rose bali ni mdogo
wake anaitwa Innocent ingawa pia aliwaza kuwa ni kwanini alikuwa speed kwa
kiasi hicho.
Tafadhali kaka unanichelesha
nyumbani, mimi naitwa salma Ramadhani ninaishi barabara ya kumi nane ni mwalimu
wa watoto wasioona akaishia hapo ‘’nashukuru kwa kuridhika tufahamiane mimi naitwa Imma salimu ni meneja kwenye
kampuni kusafirisha magogo nje ya nchi’’alijieleza kwa ufupi kijana Imma ila akawa hajaridhishwa na maelezo ya salma ikambidi amuombe wakae
sehemu ili waongee Salma alikataa kata
kata kwa madai kuwa anachelewa kurudi nyumbani Imma alijitaidi ata kumuomba
ampeleke kwake kwa gari yake lakini Salma hakuwa tayari, ‘’basi naomba japo
namba yako ya ’basi naomba japo namba yako ya simu Salma mbona unakuwa hivyo
kumbuka binadamu hufahamiana kwa namna tofauti amini hii ndio njia pekee
aloweza kutukutanisha mwenyezimungu’’ alilalamika Imma ila Salma alimjibu kuwa
hana mawasiliano mengine zaidi ya kumueleza anapoishi ikamlazimu Imma kuridhika na maelezo ya salma akaingia kwenye
gari na kurudi nyumbani huku akitamani sana kwenda kukutana na Salma kitu
ambacho aliamini kinawezekana ingawa hata ramani aliopewa isingemuwezesha
kufika akaendelea na safari ya kuelekea kwake huku akiwa na mawazo mengi juu ya
salma Ramadhani.msichana huku akitamani sna kujua miasha yake na hali ile
inatembea barabarani bila hata msaidizi “mmmhh yule dada itakuwa anaishi na
nani maskini ya mungu mmmmhh lakini Salma ni mrembo kwani mungu angempa macho
kweli ingekuwa balaa’ aliwaza Imma akiwa amejitupa kwenye coach la chumbani
kwake.
Salma alikuwa akiishi na dada
yake tu ambae hakuwa na baba wala mama kwani wote walifariki kwenye ajali gari
iliyotokea iliyoluwa ikivuka kwenye pantone ya kivukoni kwenda posta na
kupoteza maisha hapo hapo wakiwa na kaka yao na mdogo wao wa kike (mwanahuba)
ambapo walikuwa wakimsindikiza Mwanahuba shuleni Ruvu miaka sita iliyipita na kwa kipindi chote hicho alikuwa akiishi na
dada yake ambae ni mwalimu wa shule ya msingi kisosora na muda huo alikuwa
anamfuata dada yake ambapo ni kawaida yake baada yeye kutoka kazini kumfuata
dada yake ambae anafanya karibu kidogo na kazini kwake na huwa wanarudi wote,
ila hakupenda kumruhusu mwanaume amchezee mwili wake hata mara moja kwani alikuwa
akihusiwa na dada yake kila siku huku ukizingatia kuwa baada ya Wazai wao
kufariki hawakuweza kusomeshwa zaidi ya dada yake huyo alouza badhi ya mali na
kujiunga na chuo cha ualimu wa shule ya msingi na kupangiwa kisosoro mjini
Tanga kizingatia kuwa yeye ni kipofu
alifahamu kuwa hakuna mwanaume ambae angekuwa mkweli zaidi ya kumchezea na kisha
kumtupa hivyo aliapa kutompa mwanaume yoyete nafasi hata ya kusumbua ubongo
wake.
Imma aliendelea kuumiza kichwa
juu ya maisha ya Salma baada ya siku kadhaa akiwa anahangaika na picha ya Sama
ambayo haitoki kichwani mwake akiwa amepunguza baada ya kazi akiw na rafiki
yake kipenzi James Mhina, Imma akajikuta akimsimulia kile kilichomtokea
sikuchache zilkizopita huku akionesha kuguswa kwake na tukio hilo, ingawa
ilikuwa tofauti na matarajo yake kwani kwa upande wa james mambo yanakuwa tofauti
na alivyotarjia Imma ‘’my best unachekesha yaaani unaumiza kichwa juu ya binti
usomfahamu,kibaya zaidi ni kipofu na
wakati unatakiwa kunipa habari za mkeo mtarajiwa Rose sasa kipofu maisha haya
ni nin kama sio mikosi na matatizo ya maisha, fikiria Rose mtoto mwenye mvuto
halafu humtaki sasa utaishi nae vipi?hicho kitakuwa kituko’’alimaliza kwa
kuponda na kumfanya Imma amuone James kuwa
ni adui wa mawazo alikuwa nayo.
‘’Yani best unadiriki kunitamkia maneno hayo
sawa tufanye yameisha’’alilalamika Imma na kuishia kwa neNO yameisha kwani
hakuwa muongeaji sana ila roho ilimuuma sana . Kwani alikjikuta
hana mtu wa kuweza kumuelezea hisia zake za ndani na namna gani lile swala
limemgusa.
Kesho yake mida ya saa tano
mchana aliamua kwenda kumtafuta Salma huku kiwaza ‘’kwa kuwa leo ni jumamosi natumai nitamkuta
nimueleze yaliyo moyoni mwangu’’ baada ya mwendo wa dakika ishirini ndani ya
Rava 4 anawasili barabara ya kumi na na
nane akiwa hajui amuulize nani anaamua kushuka na kumuita kijana mmoja aliyekuwa
nje ya nyumba nyumba moja mbovu mbovu’’samahani namuulizia dada mmoja anaitwa
Salma Ramadhani “mmmhh hapana hapa
mtaani hakuna dada mwenye jina hilo” alijibu yule kijana jibu ambalo lilivunja
matumaini ndani ya ubongo wake,ghafla alimuona mama mtu mzima akikaribia walipo
“samahani mama anmuulizia dada mmoja hapa mtaani anaitwa salma nimlemavu wa machohuwa anatembelea na fimbo
sijui unamfahamu ‘’ Yule mama alikaa kwa muda kidogo akiwaza kisha ‘’hao wadada
wapo wawili hapa mtaani ila majina yao siwafamu mmoja ni mwalimu mwengine
anasoma sijui unamuulizia yupi? ‘’alimaliza Yule mama baada ya kusikia hivyo
Imma alianza kuonyesha tabasamu na akijikuta akijibu kwa pupa’’ huyo ambae ni
mwalimu’’yule mama alimuelekeza kuanzia pale kwenye nyumba nyeupe hesabia
nyumba ya kwanza , ya pili ya tatu ndio yao ahsante sana kijana chukua hii pesa
na mama hii itakusaidia alitoa noti
shilingi alfu tano na alfu kumi na kuwapa
‘’jamani ahsanteni ‘kisha Imma akaondoka kuelekea alipoelekezwa ‘’hodi’’ aligonga mlango mara akasikia sauti
ikimuamuru aingie.
Ilikuwa ni nyumba moja ambayo ilionekana kuwa ni ya zamani ambayo kwamba
hata mtoto anaweza kugundua kuwa ilikuweko kabla ya Tanganyika haijapata uhuru, Imma
aliingia ndani na kumkuta dada mmoja ambae hakumfahamu ila alionekana kuwa ni
mtu mzima kidogo ‘’Shikamoo dada
aliamkia Imma ‘’
‘’marahaba kijana unashida gani?aliuliza Yule dada
‘’samahani dada mimi naitwa Imma nilikuwa namuulizia dada mmoja anaitwa
Salma Ramadhani nimeelekezwa hapa sasa sijui nimemkuta?’’alimaliza kwa kuuliza
swali
‘’Salma? alishtuka Yule dada baada yakusikia kwa mara ya kwanza mwanaume
anamuulizia ila akaona asiendelee kumuhji ila amuite tu Salma na baadae afahamu
kitakacho fuata,
‘’ndio umemkuta je ukimuona utaweza kumfahamu?
‘’bila shaka kwani namfahamu vizuri zaidi,
Yule dada akaingia ndani mara
Salma alitoka huku akiwa na wasiwasi mkubwa kwani hakutarajia kitu kama hicho wewe ni nani unaniulizia na je unashida gani
na mimi?’’
mimi ni Imma
Salimu’’alijitambulisha kwa Salma lakini Salma hakuonyesha kumfahamu ‘’mbona
sikufahamu unasema unaitwa Imma?’’aliuliza swali kwa mshangao huku dada yake
akiwa anamskiliza kwa makini zaidi,ila Imma hakupenda kuona ile hali ya
kutofahamiana na mtu ambae anapenda kuwa na mahusiano nae ya karibu ,akatulia
kwa mda kisha akaendelea ‘’mimi ni Yule
dereva uliyekutana nae makutano ya barabara za kisosora na stendi juzi kabla
hajamaliza Salma alionyesha kumkumbuka
‘’ahaa ‘’sasa nimekumbuka haa yani umekuja kwetu unashida gani?aliuliza
swali huku kwa mbali akionyenya tabasamu
‘’usiwe na wasiwasi nimekuja naomba unipatie nafasi tutoke tukaongee
Salma samahani kama nitakuwa nimekosea’’alitupa ombi hilo huku akisubirikwa
Salma aongee
we kaka kwanini unakuwa sio muelewa
nimekwambia siko tayari kufanya chochote na wewe naomba naomba niache ‘’
alieleza kwa jazba kidogo kiasi cha kumfanya Imma aanze kuchanganyikiwa ‘’Salma naomba usiongee maneno hayo naomba nielewe
Salma kasha unisikilize.
‘’nimeshakwambia siwezi kwenda na mwanaume
yoyote huo ndio ukweli wangu samahani kama nitakuwa nimekosea’’dada yake alimdakia
‘’we Salma naomba uende nae msikilize huyo ni mwenzio hujui anataka kukwambia
nin?alimaliza kwa maneno hayo na kumfanya Salma aanze kutafakari na kujikuta
akiitikia ‘’sasa dada’’ ‘’sasa nini unakosa ustarabu’’baada ya
mazungumzo hayo Salma alienda ndani huku akiwaacha dada na Imma wakiwa wameduwa
wasielewe aidha amekubali au laa,baada ya kimya cha dakika kama
saba Salma alitoka akiwa amependeza kiasi cha kumfanya dada yake aanze kumtania
‘’he Salma hiyo safari ulikuwa umeshaipanga
nini?’’ila Salma hakjibu kitu alikuwa akiendelea kupapasa njia ya kutokea na
kumfanya Imma asielewe kama wanakweda au anasafari zake ‘’twende”,.Dada tutakutana baadae kama nitarudi salama’’aliamrisha huku akiambatanisha na kuaga.
Imma alimfuata na kumshika mkono hadi kwenye
gari lake wakaingia
na kuanza safari kuelekea hotel ya MK. INN ambayo ni maarufu sana jiji hapo .
Wakiwa wanakaribia MK Hotel Imma
anashangaa kuiona gari ya Mzee Martin akiwa anawaza atafanyaje kama mzee martini baba mkwe wake mtarajiwa atakuwa pale
nin kitafuata? mara kwa pembeni anaiona gari ya Rsoe ndipo akagundua familia
kuwa Familia ya Mzee martini ilikuwa hapo ikiwa ni Rose,Mama yake na Baba yake.
Mmmmmhhhhhhhhhhh hayaaaaaa
usikose sehemu ya sita
If you can't accept your wrongness you can't determine
your weakness
“mungu ndio mwanga wa maisha yetu”